Na Beatrice Kaiza
UFUNGUZI wa shindano la ulimbwende wa Miss Kinondoni 2024 wafanyika rasmi uliyoandaliwa na mrembo Queen Johnson, mlimbwende mwenye makampuni na taasisi lukiki zilizotoa fursa za ajira na ufahamu katika Jamuhuli ya Muungano akimuunga mkono Rais Samia Suluhu Hasani.
Akizungumza na waandishi wa habari Queen Jonson amesema kuwa Ulimbwende imeleta viongozi lukuki katika taifa na ajira kwa warembo mbalimbali akiwemo Jokate, na wengine wengi, imeleta hamasa kubwa kwenye ujenzi wa taasisi zisizo za kiserikari na makampuni ya kibiashara, walimbwende wamekuwa mstari wa mbele kwenye ujenzi wa Taifa letu kiuchumi na ki ustawi wa Jamii.
“Miss Kinondoni wamekuwa vinara katika mashindano mbalimbali ya ulimbwende ya Tanzania na Dunia, Kinondoni tuna kila sababu ya kujivunia kwani 2004 Faraja Kotta, 2005 Nancy Sumari, 2006 Wema Sepetu, hao ni baadhi ya walimbwende wa Kinondoni waliofanya vizuri kwenye Tasnia hii napenda kutoa wito kwa warembo kutoka sehemu mbalimbali kuja kujiunga na Miss Kinondoni 2024 ili kutimiza malengo yao,” amesema Queen.
Pia ameongezea kuwa kuhusu vigezo na masharti kwa washiriki ni kuwa karibu na mitandao yao ya kijamii ikiwemo ‘Instagram’ Miss Kinondoni 2024.