Pamoja na mambo mengine, viongozi hao wamejadiliana na kukubaliana kuongeza fursa na ushirikiano katika nyanja za mafunzo na uzoefu kwa wataalam wa pande zote mbili. Aidha, katika Utekelezaji wa mambo hayo, viongozi na wataalam wa Tanzania na Oman watakutana hivi karibuni kupanga mikakati ya utekelezaji wa makubaliano ya ushirikiano.
Mazungumzo hayo ni hatua ya utekelezaji wa Balozi wa Tanzania nchini Oman, Mhe. Fatma Rajab ya kukuza ushirikiano wa kidiplomasia na Utekelezaji wa Diplomasia ya Uchumi.