Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi (CDF) Jenerali Jacob John Mkunda amesema hali ya ulinzi na usalama Nchini ni shwari licha ya uwepo wa matishio ya kigaidi na itikadi kali ambapo Wanamtandao wa kigaidi wamekuwa wakiwalingania Vijana wenye umri wa kati va miaka 15 a 35 kisha kuwasafirisha kwenda kujiunga na vikundi vya kigaidi Nchi za DRC, Msumbiji na Somalia.
CDF Munda amesema hayo mbele ya Rais wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Dkt. Samia Suluhu leo January 22,2024 wakati wa Mkutano wa Saba wa CDF na Makamanda Jiini Dar es salaam. CDF amenukuliwa akisema "Hali ya ulinzi na usalama ndani ya Nchi kwa ujumla ni shwari licha ya uwepo wa matishio ya kiusalama hasa tishio la kigaidi na itikadi kali, Wanamtandao wa kigaidi wamekuwa wakiwalingania Vijana wetu wenye umri wa kati ya miaka 15 a 35 kisha kuwasafirisha kwenda kujiunga na vikundi va kigaidi hususani katika Nchi za DRC, Msumbii na Somalia hali inayoonesha upo ukuaji wa tatizo hilo hapa nchini."
"Dawa za kulevya, matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii na ongezekeo la Wahamiaji haramu ni miongoni mwa masuala vanayohatarisha hali ya usalama ndani ya Nchi yetu, hata hivyo matishio hayo vanaendelea kudhibitiwa kwa ushirikiano a vyombo vingine vya usalama"