Mkuu wa mkoa wa Katavi Mheshimiwa Mwamvua Mrindoko ameipongeza Tume ya Taifa ya Umwagiliaji kwa kuendelea kuboresha sekta ya umwagiliaji nchini pamoja na kuendelea kutoa elimu ya ada ya huduma za umwagiliaji kwa wakulima katika skimu za umwagiliaji nchini.
Mrindoko ametoa kauli hiyo wakati wa ziara ya Wataalamu kutoka Tume ya Taifa Umwagiliaji makao makuu iliyoongozwa na Mkuu wa Kitengo cha Sheria NIRC Bw. Andrew Rugarabamu akiambatana na wataalamu wa kada zingine, ambapo ziara hiyo ina lengo la kutoa elimu kwa wakulima umuhimu wa ada ya huduma za umwagiliaji.
Aidha Mhe. Mrindoko ameishukuru Tume ya Taifa ya Umwagiliaji mkoa wa Katavi kwa kuendelea kufanya kazi kwa ushirikiano na ofisi yake pamoja na kuendelea namchakato wa utambuzi wa maeneo yenye fursa za umwagiliaji katika mkoa huo.
Hata hivyo naye Mkuu wa Kitengo cha Sheria NIRC Bw. Andrew Rugarabamu ameeleza dhumuni la ziara hiyo ni kutoa elimu kwa wakulima umuhimu wa ada ya huduma za umwagiliaji.
Wataalamu hao wa wanataraji kufanya ziara ya utoaji wa elimu katika skimu za umwagiliaji zilizopo mkoa huo ikiwemo skimu ya Itenka, Mnyagala, Iloba, Mtapenda, Kilida na Mwamapuli.



