Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Limewachagua Mrisho mpoto na Ritha Paulsen (Madam Ritha) kuwa mabalozi wake ili kutangaza shughuli zinazofanywa na Baraza hilo kitaifa na kimataifa.


Akizungumza Leo August 15/2023 Jijini Dar es na Waandishi wa Habari Katibu Mtendaji wa BASATA Dkt Kedmon Mapana amesema kwa mujibu wa mtiririko wa utekelezaji wa shughuli za sanaa nchini Baraza limedhamiria kuwa na mabalozi watakaofanya kazi ya kutangaza majukumu ya Baraza  wanayofanya ndani na nje ya nchi.



Ameongeza kuwa Mabalozi hao watasaidia kutambulisha taasisi hiyo ambayo inayoshughulikia mustakabali wa maendeleo ya wasanii na wadau wa sanaa nchini.

"Mabalozi wetu Hawa watashirikiana na baraza la sanaa la Taifa ili kupanua wigo wa mawazo na kutangaza falsafa yetu iloyojikita katika kufufua zaidi kukuza zaidi na kuendeleza zaido sekta ya Sanaa na kuipa mawanda mapana ya ubunifu na ushirikiano huu umejikita katika makubaliano ya kufanya kazi kwa muda wa miezu 12 kuanzia leo ambapo tutasaini mkataba wa maridhiano " amesema Dkt Mapana.


Akizungumza kwaniaba ya Balozi mwenzie Madam Ritha, Balozi Mrisho Mpoto(Mjomba ) ameshukuru Basata kumwamini yeye na Madam Ritha kuwapa dhamana hivyo watajitahidi wanakututana na wasanii kurudisha maadili kwenye jamii kwani sasa nyimbo zinazoimbwa zinaendana na tamadani za Kitanzania na kupunguza nyimbo zinazoimbwa kinyume na Maadili.