Na Beatrice Kaiza
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila amefanya ukaguzi katika Soko la samaki Ferry na kuzungumza na
wafanyabishara wa samaki katika Soko iIo Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari Chalamila ameeleza nia njema ya Rais Samia kwa wafanyabishara wa soko hilo amehimiza kila mfanyabiashara kushirikiana na wenzake ii idadi ya wafanyabiashara ambayo saza ni zaidi ya 3,000 isiongezeke hadi Serikali itakapofanya maboresho ya soko.
“Nimegundua changamoto kadhaa ikiwa ni pamoja na ukosefu wa nidhamu ya biashara, kutokuwepo kwa uaminifu katika ukusanyaji wa mapato, na kutofuata sheria ipasavyo. nimemtaka meneja wa soko kuwa na ubunitu zaidi wakuongeza mapato kupitia sheria zilizoko kwa kushirikisha wafanyabiashara,” amesema Chalamila.
Pia ameagiza kupunguza matumizi ya mkaa katika soko hilo ili kupunguza uzalishaji wa moshi.
“Nimehimiza wafanyabiashara kuanza kutumia gesi ili kulinda mazingira na afya ya wote.
Aidha Chalamila amesema ujio wake katika soko hilo amebaini uholela wa Wafanyabishara, kukosekana kwa uaminifu miongoni mwa wafanyabishara kupitia kiwango cha mapato ambacho kinatakiwa kipatikane, ubovu wa miundombinu, sheria sio shirikishi hivyo ni wakati muafaka wa kuanza kupangana, pia Meneja kuwa na ubunifu zaidi katika kuongeza mapato vilevile kupitia sheria zilizoko kwa kuwa shirikisha wafanyabishara wenyewe.
Kwa upande wa Mkuu wa Wilaya ya IIala Edward Mpogolo amesema kuwa pamoja na juhudi kubwa inayofanywa na Wilaya hiyo ziko Changamoto kadhaa katika soko hilo ikiwemo migogoro kati ya zone moja na nyingine, Ukosefu wa friji la kuifadhia samaki kwa baadhi ya maeneo.
“Wafanyabiashara ni zaidi ya elfu 3, na kuwepo kwa mchanga kando ya ferry hiyo ambapo awali meli za samaki zilikuwa zinatia nanga na siku hizi haiwezekani hivyo ujio wa Mhe Mkuu wa Mkoa imekuwa faraja kubwa na wako tayari kumsikiliza na kupokea maagizo na maelekezo yake kwa masilahi mapana ya wafanyabishara katika soko hilo,” amesema Mpogolo.






