*Kufanyika viwanja vya Usagara Sekondari

*kuanzia tarehe 21 - 25 Agosti

* Waziri Ummy asisitiza umuhimu wa kila mtu kujua namba zake

Taasisi ya Afya Check kwa kushirikiana na Mbunge wa Tanga Mjini, Mhe Ummy Mwalimu a Halmashauri ya Jiji la Tanga imeandaa kambi maalumu ya wananchi kupima afya zao bure ikiwa ni sehemu ya kuunga mono jitihada za Rais Samia za kusogeza huduma za Afya kwa wananchi.






Wakiongea katika Mkutano na Vyombo vya Habari, Ukumbi wa Halmashauri ya Jiji la Tanga leo tarehe 14/Agosti 2023 Mbunge wa Tanga Mini ambae pia ni

Waziri wa Afya Mhe UMMY MWALIMU amesema kuwa Kambi hiyo itafanyika katika Viwanja vya Usagara Sekondari kuanzia tarehe 21 hadi 25 Agosti

2023.



Huduma zitakazotolewa ni kupima Pressure (Shinikizo la Damu), Kisukari, Macho a kupima aina tatu za Saratani ambazo ni Saratani ya matiti, saratani ya Mango wa Kizazi na Tezi Dume. Kuhusu kupima Tezi dume Mhe Ummy amewataka wanaume kutoogopa kwa kuwa kipimo kitakachotumika ni rafiki.

Aidha, Mhe Ummy ameeleza kuwa ni muhimu kila mwananchi kujua namba zake kuhusu uzito, Shinikizo la Damu na Sukari ili kujikinga na kudhibiti magonjwa yasiyo ya kuambukiza. Pia Kupitia kambi hii wananchi watapata huduma za kupima UKIMWI, TB a Malaria sambamba na kupatiwa dawa.



Mkurugenzi wa Afya Check Dkt ISAAC MARO @drisaacmaro ameeleza kuwa Taasisi ya Afya Check inaendesha kambi hizi ili kuwaiendea wananchi