Kamati ya Usalama Barabarani mkoa wa Iringa, imepanga kufunga Kamera za usalama kwenye maeneo korofi ambayo yamekuwa na matukio ya ajali za mara kwa mara, ikiwemo Mlima Kitonga na eneo la Changarawe maarufu "Majinja" kwa lengo la kuwa na usimamizi wa saa ishirini na nne na kukomesha kabisa ajali kwenye maeneo hayo.
Kamati hiyo imefanya ziara ya siku mbili kutembelea maeneo yenye matukio ya ajali za kujirudia kwa lengo la kuainisha changamoto za maeneo hayo ili kubainisha hatua za kuchukua na kudhibiti ajali hizo.

