Spika wa Bunge na  Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini Dkt Tulia amewashanga watu wanaosema alimtelekeza mume wake wakati wa kampeni za kugombea bunge na hata alivoipata nafasi hiyo.


Dkt Tulia amesema mume wake sio mwanasiasa hawezi kumpandisha majukwaani na anayemtaka kumuona anamtaka wa nini?



Dkt Tulia amesema hayo alipotembelea shule ya wasichana ya St Fransis na wanafunzi hao kupata nafasi ya kumuuliza maswali ambapo walihoji anamudu vipi kuchafuliwa jina lake kwa sababu ya mambo ya kisiasa.


Katika hatua nyingine Dkt. Tulia amewataka Wanafunzi wa shule hiyo kuzingatia masomo na kutanguliza nidhamu katika kila jambo ili waweze kuyafikia malengo yao kwakuwa elimu ndio msingi mkuu wa Maisha yao.