Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Hassan Abbasi leo Mei 19, 2023 akiwa ameambatana na Menejimenti ya Wizara hiyo amefanya ziara ya kukagua ujenzi wa jengo jipya la Wizara ya Maliasili ambalo linatarajiwa kukamilika Juni 30, mwaka huu.
Akiongea mara baada ya kukagua jenho hilo Dkt. Abbasi amemsisitiza Mkandarasi wa jengo hilo kutoka kampuni ya LI Jun Construction kuwa tarehe ya makabidhiano iko palepale na hakuna kitakachobadilika.
“Tarehe 30 Juni tunataka mtukabidhi jengo, msilete visingizio kazi ifanyike bila kukwama na sisi Wizara tutahakikisha tunawapatia kila mnachohitaji ili kukamilisha ujenzi kwa wakati”
Jengo hilo linalogharimu takribani shilingi Bilioni 16 litakuwa miongoni mwa majengo ya awali kabisa kukabidhiwa miongoni mwa
majengo ya Serikali yanayoendelea kujengwa katika Mji wa Serikali Mtumba Jijini Dodoma.

