STAA wa Muziki wa Bongo Fleva Nassib Abdul ‘DiamondPlatnum’ ametembelea shamba la mafunzo la Vijana wa mradi wa BBT la Bihawana Mkoani Dodoma
Katika ziara hiyo Diamond amesema kuwa amefirahishwa na vijana hao kujitokeza kwenye sekta hiyo na anaamini miaka ijayo kutakuwa na wakulima wengi amba ni matajiri
Aidha Diamond amesema ametembelea mradi huo ili kujifunza ambapo mipango yake ya baadaye anategemea kufanya kilimo
"Mimi nataka kufanya kilimo na nimekuja hapa kujifumza na baada ya hapo nitakuwa mkulima Bora"amesema Nassib Abdul
Diamond amejionea shughuli mbalimbali za kilimo katika mashamba ya Bihawana yenye ukubwa wa hekari 25 ambazo zinazofanywa na vijana hao wa mradi wa BBT wapatao 72




