Takwimu zinaonesha watumiaji wa intaneti, wameongezeka kutoka milioni 29.9 mwezi Aprili, 2022 hadi kufikia Milioni 33.1 mwezi Aprili, 2023 sawa na ongezeko la asilimia 10.7.


Takwimu hizo zimetolewa na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye wakati akiwasilisha bungeni jijini Dodoma makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Habari, Mawasiliano na teknolojia ya habari kwa mwaka wa fedha 2023/24.


Sambamba na hilo laini za simu zilizosajiliwa, zimeongezeka kutoka milioni 55.7 mwezi Aprili, 2022 hadi kufikia milioni 62.3 mwezi Aprili, 2023 sawa na ongezeko la asilimia 11.8.