Wizara ya ujenzi na uchukuzi Prof. Mbarawa akisoma hotuba ya bajeti ya Wizara
Udhibiti wa Huduma za Usafiri kwa Njia ya Anga
44. Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) imeendelea kutoa huduma za udhibiti wa usafiri wa anga, viwanja vya ndege, masuala ya kiusalama na kiuchumi katika huduma za usafiri wa anga pamoja na kutoa huduma za uongozaji ndege katika viwanja 14 nchini. Utendaji na utekelezaji wa miradi ya Mamlaka ya Usafiri wa Anga unaonyeshwa katika kitabu cba hutuba ya bujeti kuanzia ukurasa wa 95 hadi 100.
Huduma za Viwanja vya Ndege
45. Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) ina jukumu la kusimamia, kuendesha, kuboresha na kuendeleza viwanja vya ndege 58 vinavyomilikiwa na Serikali.
46. Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia TAA imekamilisha maandalizi ya mahitaji ya kiufundi na ununuzi wa kandarasi kwa ajili ya ujenzi wa majengo ya abiria katika viwanja vya ndege vya Mpanda, Songea, na Kahama. Pia. imeanza maandalizi ya ujenze wa Jengo la Waongoza Ndege katika Kiwanja cha Ndege Bukoba. Pia TAA imeanza matayarisho ya ukamilisha wa ujenzi wa Jengo la Abiria wa Kiwanja cha ndege cha Mwanza.
