Kama ilivyo ada na shauku yangu kwa miaka mingi sasa tangu mwaka 1992, nimekuwa mfuatiliaji wa siasa ushindani katika nchi hii.
Kwa sasa shauku yangu kuu, iliyodumu kwa zaidi ya miaka 20 imekuwa kuisoma na kujifunza kila wakati kuhusu Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).
Lazima niwe mkweli, shauku hiyo kwa kiwango kikubwa ilijengwa na maneno aliyosema Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere kuhusu Chadema kabla ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 1995. Sina sababu ya kuyarejea, hapa kwa sasa.
Sababu kuu ya pili ya kuifuatilia Chadema iliendelezwa kwa kiasi kikubwa na kazi aliyoanza kuifanya Freeman Aikaeli Mbowe katika kipindi cha kati ya mwaka 2000 na 2005 alipokuwa Mbunge wa Hai kwa tiketi ya chama hicho, hata kabla hajachaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Chadema mwaka 2004.
Sababu ya tatu ya shauku yangu ilijengwa katika misingi ya kukatishwa kwangu tamaa na kuharibika na kuharibiwa kwa kazi ya kutukuka iliyoanza kufanywa na viongozi wakuu wa mwanzo wa mageuzi nchini akina Mabere Marando, Dk. Masumbuko Lamwai, James Mbatia, Ndimara Tegambwage na wenzao kadhaa ndani ya chama cha NCCR Mageuzi.
Kwa sababu ya shauku hiyo, kila wakati nimekuwa nikipatwa na mhemuko mkubwa wa kifikra na pengine hamasa ya kujiingiza katika minyukano ya kichambuzi ninapoona kuwapo kwa jitihada za baadhi ya mashujaa wapya wa demokrasia wakifanya mashindano yanayofanana na ujinga uliopata kufanywa na waasisi wa mageuzi nchini ambao wala sipati shida kuandika tena leo, ndiyo umekuwa mpenyo na turufu ya CCM kubakia madarakani.
Katika kufanya hivyo, mara kadhaa nimejitahidi kuikana nafsi yangu, hata kujaribu kujitwika 'magunia ya misumari kichwani' ilimradi tu nifanye kile ninachoamini kinaweza kunusuru ustawi wa demokrasia shindani nchini.
Ni kwa sababu hiyo basi ndiyo maana nimeona ni busara leo kuipa Chadema 'ole' kwa sababu ya kile ninachokiona kikiendelea kutokea ndani ya chama hicho.
Kwa namna ile ile ilivyopata kuwapo kabla, nachelea kuandika kuiasa Chadema kukwepa mtego wa kiburi na jeuri ya mafanikio...gusa link kwenye BIO yetu kusoma zaidi.

