Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa amesema, Serikali imepanga kuendelea na ujenzi wa viwanja vipya vya ndege vya Geita, Simiyu na Msalato.
Aidha, wizara imepanga kufanya ukarabati, upanuzi na uboreshaji wa viwanja vya ndege 20 nchini ambavyo ni pamoja na viwanja vya ndege vya Kigoma, Mpanda, Tabora, Songwe, Mwanza, Arusha, Mtwara, Sumbawanga, Shinyanga, Iringa, Musoma, Songea, Dodoma, Tanga, Lake Manyara, Lindi, Moshi, Bukoba, Julius Nyerere (JNIA) na viwanja vingine vya ndege vya mikoa.

