-
Wizara ya ujenzi na uchukuzi Prof. Mbarawa akisoma hotuba ya bajeti ya Wizara.
Waziri amesema Mheshimiwa Spika, Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi mahiri wa Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeweza kupiga hatua kubwa ya mafanikio katika eneo la ujenzi wa barabara na madaraja.
Katika kipindi chake cha miaka miwili wa uongozi wa Mheshimiwa Rais, barabara katika maeneo mbalimbali zimejengwa na kukamilika. Barabara hizo ni pamoja na:-
i).Barabara ya Loliondo – Mto wa Mbu (km 201); Sehemu ya Waso – Sale Jct (km 49) mkoani Arusha;
ii).Barabara ya Morocco – Mwenge (km 4.3) kutoka Njia tano hadi Sita (km 3.2) Mkoani Dar es Salaam;
iii).Barabara ya Kongwa Jct – Mpwapwa – Gulwe – Kibakwe (km 98); Sehemu ya Mbande – Kongwa Jct (km 5.80) Mkoani Dodoma;
iv).Barabara ya Tabora – Koga – Mpanda; Sehemu ya 3: Kasinde – Mpanda (km 108) pamoja na kipande cha Barabara ya Urwira (km 3.7) Mkoani Katavi;
6

