12. Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2022/23, Sekta ya Ujenzi ilitengewa jumla ya Shilingi Bilion 44.293 kwa ajili ya Matumizi ya Kawaida. Hadi Aprili, 2023 jumla ya Shilingi Bilion 32.893, sawa na asilimia 74.26 ya fedha zilizoidhinishwa na Bunge zilikuwa zimetolewa kwa ajili ya Matumizi ya Kawaida.
Bajeti ya Miradi ya Maendeleo
13. Mheshimiwa Spika, kwa upande wa miradi ya maendeleo, katika mwaka wa fedha 2022/23, Sekta ya Ujenzi ilitengewa Shilingi Trilioni 1.377. Kiasi hicho kinajumuisha Shilingi Trilioni 1.124 fedha za ndani na Shilingi Bilioni 252.965 fedha za nje. Fedha za ndani kutoka Mfuko Mkuu wa Serikali (Consolidated Funds) ni Shilingi Bilioni 777.785 na kutoka Mfuko wa Barabara ni Shilingi Bilioni 599.756.
Hadi Aprili, 2023 fedha zilizopokelewa ni Shilingi Trilioni 1.312 sawa na asilimia 95.3 ya fedha zilizoidhinishwa kwa mwaka wa fedha 2022/23. Kati ya fedha hizi, Shilingi Trilioni 1.069 ni fedha za ndani na Shilingi Bilioni 243.321 ni fedha za nje.
14. Mheshimiwa Spika, nitumie fursa hii kuipongeza na kuishukuru sana Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kulipa hati za madai ya Makandarasi na Washauri Elekezi kwa wakati."

