Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kwa mara nyingine tena amewaomba Wafanyabiashara wa Kariakoo wakubali kufungua maduka yao ili biashara iendelee kama kawaida ambapo amesema Kamati iliyoundwa leo yenye uwakilishi wa Wafanyabiashara pia itahakikisha malalamiko yote yanafanyiwa kazi.


Baada ya ombi hilo la Waziri Mkuu Wafanyabiashara wameonekana kukubali kwa kupiga makofi huku wakiahidi kufungua maduka.



Waziri Mkuu amesema “Naomba mrudi mkaendelee na biashara, makofi haya ni ishara kwamba mmeridhia kwenda kufungua biashara ikiwezekana hata leo na kwakuwa Rais Samia anafuatilia naomba makofi yaongezwe “