Mkurugenzi na Muandaaji wa Maonesho Deogratius John Kilawe awataka watanzania kujitokeza katika maonesho ya Dar es Salaam Constuctions Expo ili kujifunza Teknolojia mpya itakayopatikana katika sekta ya ujenzi.


Akizungumza na waandishi wa habari leo 10 Oktoba 2023, Jijini Dar es Salaam katika Ukumbi wa Diamond Jubilee  amesema kuwa Maonyesho hayo  yamejikita kwa lengo la kuwakutanisha pamoja wadau wa sekta ya Ujenzi na kujadili njia mbalimbali zitakazosaidia kuinua sekta hiyo pamoja na kukuza mahusiano na kujipatia  wateja wa Bidhaa zao.


“Maonesho hayo ni kuanzia  Tarehe 11- 13  Oktoba 2023  na kufanyika katika  Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dae es salaam wadau mbalimbali na Watanzania tunaomba wajitokeza kwa wingi katika maonesho hayo ili kujifunza Tsknolojia mpya itakayopatika na  katika sekta ya Ujenzi,” amesema  Kilawe.


 Aidha aliongezea kuwa, huu ni msimu wa 7 wa  Maonesho ya Dar Constuctions Expo na   yanajumuisha zaidi ya  Makampuni  120 kutoka nje na ndani ya Tanzania pia yanatarajiwa kuwa yenye kuleta Tija na Mapinduzi katika sekta ya ujenzi  na kukuza na kuendeleza Uchumi wa nchi pamoja na Kuchangia Pato la Taifa.


Pia amesema kuwa kutakuwa na na Makampuni ambayo yatasaidia Watanzania kupanua wigo mpana wa Uzalishaji wa bidhaa  zenye ubora wa kiwango cha juu zitazoleta Ushindani katika Soko la Kimataifa.