Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utali Mhe.Benedict Wakulyamba amelipongeza Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) kwa uhifadhi uliotukuka na usio na mashaka kwa taifa.

Kamishna Wakulyamba ameyasema hayo leo tarehe10.10. 2023 alipotembelea Hifadhi ya Taifa Kitulo ilivopo wilayani Makete katika mkoa wa Njombe.

Ndani ya hifadhi hiyo Kamishna Wakulyamba alitembelea Lango la Mwakipembo, Uwanda wa Maua, Maporomoko ya maji ya Mwakilema na Mwakipembo.

Baada ya kuviona vivutio hivyo a baadhi ya mamalia wachache walioonekana kwa muda huo, hakusita kuonesha furaha yake alipotazama upande wa

Mashariki na kuona mandhari nzuri iliyonakshiwa kwa safu za milima ya Livingstone a tambarare iligotaradadi kwa maua yenye rangi tofauti mithili ya zulia.



"Nimeridhishwa na kazi nzuri za uhifadhi mnazozifanya maafisa na askari wa TANAPA.



Hongereni kwa kuendelea kuhifadhi rasilimali zetu, serikali na wizara inatambua kazi nzuri mnayoifanya ya uhifadhi kwani mnajituma usiku na mchana."

Kwa tafsiri isiyo rasmi mwanamapinduzi kutoka chini

India Mahatma Gandhi aliwahi kusema, Utajiri wa taita lolote lile duniani unategemeana na jinsi taifa hilo linavyoheshimu a kulinda wanyamapori wake.

Hivyo wanachokifanya TANAPA ni kuendeleza falsafa

hiyo.