Mmiliki wa mtandao wa zamani Twitter, Elon Musk, amesema hivi karibuni mtandao huo, utaongeza kipengele cha kupiga simu kwa njia ya sauti na video. Elon ametoa taarifa hiyo, kupitia mtandao huo, ambapo amebainisha kuwa kipengele hicho, kitapatikana kupitia ioS, Android, Mac and Windows na hakitamuhitaji mtu kutumia namba ya simu.