Mkurugenzi wa Taasisi ya
Nasimama na
Binti Wema Sepetu ameahidi
kutoa
madawati 50 kwenye Shule tatu alizotembelea
Wilayani Pangani Mkoani Tanga ambapo amegawa pia zawadi mbalimbali katika
Shule hizo zikiwemo jezi, daftari pamoja na kalamu ili
kuwasaidia Wanafunzi hao kusoma kwa bidii na
kusaidia uboreshaji wa elimu.
Wema ametoa ahadi hiyo baada ya yeye pamoja
na Mkuu wa Wilaya ya Pangani Zainab Abdallah pamoia na watu wengine
akiwemo Msanii Maarifa walipotembelea na kuongea
na Wanafunzi wa Shule za Sekondari Kipumbwi na
Mwera, Bushiri, Kimanga zilizopo Wilayani Pangani.
Kwa upande wake DC Zainab amesema
wametembelea Shule hizo katika mendelezo wa
kampeni ya Niache nisome Pangani inanitegemea
ambayo inalenga kuhamasisha
ukuaji wa elimu Pangani, kampeni hiyo itahitimishwa
kesho na itahudhuriwa na Viongozi mbalimbali.
Akiongea na Wanafunzi hao DC Zainab amesema
"Mnapaswa kuongeza bidii kwenye elimu ili
mufanikiwe zaidi na kutimiza ndoto zenu, tuna
Viongozi wengi Vijana kwenye Nchi yetu, walisoma
na ndio maana wamefika hapa, niwaombe muweke
msukumo mkubwa kwenye masomo yenu ili tuwe na
Taifa lenye wasomi wengi"







