Ziara ya kamati ya utekelezaji ya UVCCM Taifa inayoongozwa na Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Ali Kawaida ambayo imeanza tarehe 11 Agosti 2023 imezaa matunda kwani imetatua changamoto nyingi za vijana nchini
Moja ya changamoto ambazo UVCCM wamezitatua ni kuhakikisha vijana Waendesha bodaboda wanapewa kibali cha kupewa maeneo yenye mkusanyiko ya watu lakini pia kuekewa sheria rafiki ambazo zitaweza kuwasaidia waweze kufanya shughuli zao kwa usalama ili waweze kujiingizia kipato na kupelekea kuchangia Pato la Taifa.
Akizungumza na waandishi wa Habari Jana Jijini Dar es Salaam, Katibu Idara ya Uhamasishaji na Chipukizi(UVCCM),Taifa, Edna Lameck amesema ziara hiyo itakwenda nchi nzima na tayari wameshaingia katika mkoa wa Dar es Salaam katika Wilaya zake zote 5.
Aidha amesema katika ziara hiyo wamekutana na makundi mbalimbali ya vijana na kuongelea namna gani serikali imeendelea kuwagusa vijana hasa kwenye mfuko wa asilimia 10 ambapo vijana, wanawake na watu wenye Ulemavu wananufaika.
“Ziara hii ilianzia Zanzibar katika eneo la unguja na tumetembelea takribani mikoa yote minne na Wilaya zake zote, ni ziara nzuri na imezaa matunda makubwa ambapo lengo la ziara hii hasa ni kukutana na makundi mbalimbali ya vijana wa kitanzania ambao wanajishughulisha na shughuli nyingi za kimaendeleo lakini pia kuhakikisha wanailetea tunu ya Taifa maendeleo” Amesema Edna
Amesema Jumuhiya ya Vijana wa Chama Cha Mapinduzi imekabidhiwa jukumu la kuwasemea na kuwasaidia vijana wote wa kitanzania walio na vyama na wasio na vyama.
Mbali na hayo Edna amesema leo terehe 27 watakuwa na mkutano mkubwa wa hadhara utakaofanyika katika viwanja vya mbagala zakhiem jijini Dar es Salaam wenye lengo la kuzungumza na umma wa watanzania hasa vijana wapenda maendeleo wote juu ya namna serikali inaendelea kujitahidi kuwasaidia vijana hasa katika pande zote ikiwemo, elimu, afya, ajira lakini pia kuendelea kujiajiri katika maeneo mbalimbali
Pia amesema mkutano mkutano huo utalenga kuwaeleza vijana namna serikali inavyoendelea kuleta maendeleo nchini.
“Nawakaribisha watanzania wote katika viwanja vya dar es salaam, saa 7 mchana ambapo watu mbalimbali mashuhuri watakuwepo na viongozi mbalimbali watakuwepo”