Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb.) amewapa Wakuu wa Mikoa mbinu mbalimbali za kutekeleza Diplomasia ya Uchumi katika Mikoa yao.


Dkt. Tax ametoa mbinu hizo tarehe 26 Agosti, 2023 wakati wa Mafunzo ya Uongozi kwa Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa yanayofanyika katika Shule ya Uongozi ya Mwalimu Nyerere iliyopo Kibaha mkoani Pwani.



“Mbinu za kuibua na kutekeleza diplomasia ya uchumi ni nyingi kama vile kufungua balozi, kukusanya taarifa na uchambuzi, majadiliano,……………….lakini kwenu nyie Wakuu wa Mikoa mnaweza kufanya makongamano ya biashara na uwekezaji na kuzitangaza fursa mbailmbali za biashara katika mikoa yenu pamoja na elimu kwa Umma,” alisema Dkt. Tax.


“Kupitia mikoa yenu mnaweza mkafanya makongamano ya biashara na uwekezaji na kuzitangaza fursa za biashara katika mikoa yenu, ninyi ni wadau wakubwa wa kutekeleza diplomasia ya uchumi kwa vitendo na kuchangia maendeleo,” alisema Dkt. Tax


Alisema kuwa Serikali itaendelea kuboresha  mifumo ya sheiria, kiutendaji na kukuza mazingira ya kushindana Kimataifa na Ofisi za Wakuu wa Mikoa zina mchango mkubwa kufanikisha utekelezaji wa Diplomasia ya Uchumi na hivyo kuchangia maendeleo ya kiuchumi nchini.


“Serikali itaendelea kuboresha mifumo ya kisheria, kiutendaji na kukuza mazingira wezeshi kushindana kimataifa ambapo ofisi za wakuu wa Mikoa zina nafasi na mchango mkubwa wa kufanikisha utekelezaji wa Diplomasia ya uchumi, na kuchangia kasi ya maendeleo nchini,” alisema Dkt. Tax. 


Waziri Tax aliongeza kuwa Wakuu wa Mikoa ni wadau wakubwa katika kutekeleza diplomasia ya uchumi kwenye mikoa yao kwani huibua fursa mbalimbali za biashara na uwekezaji zinazopatikana katika mikoa yao.



Pamoja na mambo mengine Waziri Tax aliongeza kuwa ofisi za Wakuu wa Mikoa ni wadau muhimu na wanalo jukumu la kibua fursa katika maeneo yao kama Mamlaka za msingi zinazobuni mipango ya biashara, miradi ya uwekezaji, uzalishaji, na utumiaji wa rasilimali katika ngazi ya mikoa.



Mafunzo ya Uongozi kwa Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa katika Shule ya Uongozi ya Mwalimu Nyerere, Kibaha mkoani Pwani yalianza tarehe 21 – 28 Agosti, 2023.