Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura), imetangaza bei mpya za mafuta zitakazotumika kwa mwezi mzima, kuanzia leo Jumatano Agosti 2, 2023 ambazo zinaonyesha kupanda kwa nishati hiyo, ukilinganisha na bei ya mwezi uliopita wa Saba.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ewura inaonyesha Kwa Mkoa wa Dar es Salaam, mafuta ya petroli yamepanda kwa Sh443 huku yale ya dizeli yakipanda kwa Sh391.
Hii inamaanisha kuwa kwa mwezi Agosti, watuamiaji wa bidhaa hizo mkoani Dar es Salaam, sasa watanunua petroli kwa Sh3, 199 huku dizeli ikununuliwa kwa Sh2, 544.
Ewura imetaja sababu za kupanda kwa bidhaa hizo kuwa ni pamoja na changamoto za upatikanaji wa dola, mabadiliko ya sera za kikodi, kushuka kwa thamani ya shilingi dhidi ya dola, na ongezeko la gharama za mafuta katika soko la dunia pamoja na gharama za uagizaji wa mafuta.


