Na Beatrice Kaiza 


SHIRIKA la Madini la Taifa (STAMICO) 

limefanikiwa kuongezeka kwa mapato ya ndani 

kutoka sh. Bilioni 1.3 kwa Mwaka 2018/19 hadi sh. Bilioni 61.1 kwa mwaka 2022/23 

ambalo ni ongezeko la asilimia zaidi ya 4,425


Kwa miaka mitatu iliyopita Shirika lilikuwa 

linakusanya kutoka vyanzo vya ndani sh. 

Bilioni 1.3 kwa mwaka, ambapo wakati huo 

huo lilikuwa linachukua ruzuku sh. Bilioni 3.4 

Hayo yalisemwa na Mkurugenzi Mtendaji 

wa STAMICO, Dkt. Venance Mwasse, wakati akizungumza na wahariri wa vyombo vya 

habari, jana Jijini Dar es Salaam kuhusu 

utekelezaji wa shughuli za shirika hilo.



Dkt. Mwasse alisema tangu kuanzishwa kwa 

shirika mwaka 1972, halikuwahi kupeleka kitu 

chochote serikalini, ambapo kwa sasa tangu 

wapate mafanikio shirika limefanikiwa kulipa 

gawio serikalini sh.Bilioni 8.


Aidha Dkt. Mwasse alisema shirika 

limefanikiwa kupata hati safi kwa miaka 3 

mfululizo kutokana na ukaguzi wa mahesabu.




Pia alisema wamefanikiwa kupata kandarasi za uchorongaji, ambapo kwa mwaka huu Aprili wamefanikiwa kusaini mkataba wenye thamani 

ya sh. Bilioni 55.2

Pia Dkt. Mwasse alisema pamoja na kulipa gawio na kuhudumia makundi maalumu, kwa 

mwaka huu wamefanikiwa kuwekeza kwenye miradi yao kwa kiasi cha sh. Bilioni 17.8 


Mbali na hayo Dkt. Mwasse alisema 

 wamefanikiwa kupata leseni mpya 6 zikiwemo 

4 za madini ya Kimkakati za lithium, Graphite 

,REE na Copper. 


Kuhusu mipango yake ya baadae, Dkt. Mwasse alisema shirika hilo limejipanga Kuimarisha uchimbaji mkubwa wa makaa ya mawe, kuongeza uwekezaji wake kwenye tasnia ya uchorongaji, kuendeleza leseni za Shirika na kuzitangaza kwa lengo la kupata wawekezaji wa madini ya ya kimkakati