Na Beatrice Kaiza 

Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama amesema anachukizwa na baadhi ya watu wanaomkashifu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suruhu Hassani kupitia mitandao ya kijamii, huku akitoa wito kwa Mamlaka husika kuwachukulia hatua watu wote wanaofanya vitendo hivyo.



Amesema kuwa watanzania wanapaswa kumheshimu

Mhe. Rais Dkt. Samia, kwani Mwenyezi Mungu ametupa mtu ambaye anaendelea kufanya kazi vizuri kwa manufaa ya Taifa la Tanzania.



"Waache mara moja kumkashifu Mhe. Rais kutokana na kwamba amekuwa anafanya kazi vizuri ili kuhakikisha uchumi wa chi unaendelea kumarika, Mhe. Rais ni Mama wa familia kama alivyo mzazi wako, tuache kutoa kauli ambazo sio rafiki" Zinazomdhihaki Rais Dkt. Samia amesema  Msama.



Aidha Msama ametoa pongezi kwa kamati kuu ya chama cha Mapinduzi (CCM) kwa kutoa elimu ya uwekezaji kwa watanzania.