Banki ya CRDB  wameingia ushirikiano na kampuni ya Samsung Tanzania utakaokuwezesha kurudishiwa 10% ya bei kila unaponunua simu mpya aina ya Galaxy Z Fold5 na Galaxy Z Flip5. na kulipia na TemboCard. 



Ushirikiano huu umetangazwa leo jijini Dar es Salaam na Mkuu wa Huduma za Kadi wa Benki ya CRDB,Bw. Farid Seif aliyeambatana na Mkuu wa Kitengo cha Simu cha Samsung Tanzania, Bw. Mgope Kiwanga mbele ya waandishi wa Habari.