Mfanyabiashara wa madini aliyetambuliwa kwa jina la Festo Marwa (55) na mtoto wake John Marwa wameuawa kikatili kwa kupigwa kichwani na kitu kizito chenye ncha kali.


Marwa na mwanawe ambao ni wakazi wa Kunduchi jijini Dar es Salaam, wamekutwa na umauti wakiwa katika kitongoji cha Mkerema Kijiji cha Lilondo, Halmashauri ya Wilaya ya Madaba mkoani Ruvuma.


Akitoa taarifa ya mauaji hayo jana Jumatano Agosti 30, 2023, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, ACP Marco Chilyaakati amesema John (mtoto) amekutwa na jeraha kubwa kichwani na uchunguzi wa awali unaonyesha kapigwa na kitu kizito chenye ncha kali kilichosababisha bongo kutoka nje.


"Baada ya mauaji hayo, wauaji hao walichukua mili yao na kuweka kwenye gari la Marwa ambalo ni Jeep kisha wakalisukuma gari hilo hadi kwenye korongo," alidai kamanda huyo.



Amedai lengo la kulisukumia gari hilo korongoni ni kutaka ionekane kuwa walipata ajali.

Hata hivyo, Kamanda Chilyaakati amesema makachelo walipolikagua gari hilo halikuwa limepata ajali.

"Baada ya kufanya utafiti tumefanikiwa kumkamata dereva aliyekuwa akiliendesha lie gari aliyetuambia kuwa baada ya tukio wenzake walimsindikiza hadi kituo cha mafuta kusudi aende polisi akatoe taarifa kwamba kapata ajali," alidai kamanda Chilyaakati.


Dereva alikutwa akiwa anakwenda polisi akatoe taarifa kwamba amepata ajali na kwenye mguu wake alipigwa na na kitu chenye ncha kali ili  naye aonekane kama amepata ajali.

"Na baada ya kumkata Dereva na kumuhoji alimtaja mtuhumiwa mwingine naye tumemkamata na wote wawili wamekiri kuhusika na hilo tukio.

"Hawa Watuhumiwa wawili ambao wote wanatoka

Kunduchi Dares Salaam wanafahamiana vizuri na marehemu na waliondoka na marehemu Agosti 27, 2023 kuja Songea wakaenda mpaka kijiji cha Amani Makolo ambako marehemu alikuwa na Vitalu 10 vya madini ya Safaya na alifanikiwa kupata Mwekezaji.

"Lakini  aliye kuwa anasaidia na kuwezesha kupatikana kwa Mwekezaji ni huyu muuwaji, marehemu alitakiwa apate 30% ya hisa katika mradi huo, lakini kwakuwa kila kitu kilikuwa kinaratibiwa na huyu muuwaji baada ya hapo mtuhumiwa huyu wa mauji alimshauri marehemu waende mbeya ambako kulikuwa na Mazungumzo ya madini.