KIKAO cha mawaziri wa sheria na wanasheria wastaafu na waliopo madarakani kimewakutanisha viongozi mbalimbali hii leo August 28 jijini Dar es Salaam kwenye majadiliano ya katiba mpya na mkakati wa elimu ya Katiba ya Tanzania ya mwaka 1977 kwa umma (MTEKU 2023/2026).
Waziri Katiba na Sheria, Ndumbaro amesema zaidi asilimia 50 ya watu hawajui katiba ya nchi huku akieleza wanajukumu la kuendelea kutoa elimu kwa wananchi juu ya Katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania.
Aidha, hayo yamesemwa kwenye kikao cha mawaziri wa sheria na wanasheria wastaafu na waliopo madarakani uliofanyika leo August 28 Jijini Dar es salaam,na kutolea ufafanuzi kwa baadhi ya watu ambao wanaodai katiba mpya kwani wameshaunda kamati ambayo itafanya mchakato wa katiba mpya.
Waziri mstaafu Mary Nagu, amesema wananchi wanapaswa kujua katiba kikamilifu ikiwemo katiba ya mwaka 1977 na kujua kitu gani kimepungua na kipi kimezidi endapo watafanya mabadiliko katika katiba mpya na kama kuna mabadiliko yafanyike na sio kuleta katiba mpya kila wakati.