-

Yanga Sc imechapwa goli 2- 1 katika mzunguko wa kwanza fainal za CAFCC.


Mechi ya fainali ya kombe la Shirikisho Afrika, kati ya Yanga na USM Algers umepigwa leo Mei 28, 2023 katika Dimba la Mkapa, Dar es Salaam.


USM Alger walikuwa wa kwanza kuona mlango wa Yanga Dk ya 30 huku Yanga wakimiliki mchezo kwa 59%


Kipindi cha Pili Yanga kupitia mchezaji wake top score wa michuano hiyo Fiston Mayele akasawazisha dk ya 81 na kabla kumeza mate USM Alger wakaongeza goli la pili 


Mechi ya leo imegubikwa na changamoto ya uwanja kuwa na maji kutokana na mvua ambayo imenyesha katika jiji la Dar es Salaam.


Mechi hiyo ya mzunguko wa kwanza uliambatana na hamasa ya Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan  kununua tiketi 5000


Mechi ya marudiano Algeria itatabiri kama Yanga wataweza kuandika  historia mpya kwenye soka la Tanzania.