Yanga wamezindua kauli mbiu ya 'WHY NOT US TUKUTANE KWA MKAPA' kuelekea katika mechi yao ya mchezo wa fainali ya Shirikisho Afrika dhidi ya USM Alger.


Mkuu wa Habari na Mawasiliano wa Yanga,  Ali Kamwe ametangaza kauli mbiu hiyo na kusema kuwa walikuwa wa changamoto ya kupata kauli mbiu hii kuelekea katika mechi hiyo itakayochezwa Mei 28 Uwanja wa Benjamin Mkapa.


“ Haikuwa jambo rahisi kuipata hii kauli mbiu maana kila mmoja alikuwa na shauku kubwa, lakini nashukuru tumeweza kuipata na katika mchezo wetu na USM Alger tutaingia na kauli mbiu ya WHY NOT US TUKUTANE KWA MKAPA” alisema Kamwe