RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ametoa ndege aina ya Bombadier kwa ajili ya kuusafirisha mwili wa Mtoto wa Waziri Mkuu mstaafu John Samuel Malecela, William Malecela maarufu kwa jina la Lemutuz
Akizungumza Mei 15, 2023 mbele ya waombolezaji waliojitokeza kumuaga mwili wa marehenu Lemutuz katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaaam, Mshereheshaji wa shughuli hiyo(MC) Hajji Manara amesema Serikali inayoongozwa na Rais Samia imetoa ndege kuusafirisha mwili wa Lemutuz.
Amesema ndege ambayo imetolewa na Serikali ina uwezo wa kubeba abiria 70 na kitendo cha Serikali ya Rais Samia kutoa ndege hiyo inaonesha inatambua mchango wake ambao ameutoa kwa jamii ya Watanzania.
"Tunampongeza Rais wetu Mama Samka Suluhu Hassan kwa kutoa ndege aina ya Bombadier kuusafirisha mwili wa Lemutuz, tunafahamu Lemutuz licha ya kuwa ni mtoto wa Waziri Mkuu mstaafu mzee John Malecela lakini inaonesha kuwa Serikali inathamini mchango wa Lemutuz katika kutoa mchango wake kwa jamii, " amesema Manara.
Kwa upande wake Meya wa Jiji la Dar es Salaam amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa usafiri wa ndege kumsafirisha Lumetuz."Tunamshukuru Rais Samia kwa kuendelea kuonesha utu wake kwa Watanzania, tunamshukuru kwa kutoa usafiri kumsafirisha ndugu yetu Lemutuz."



