Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ameagiza kuondolewa kikosi kazi cha Mamlaka ya Mapato Tanzania ambacho kinakusanya kodi kwa wafanyabiashara katika Soko la Kariakoo huku akisema ni kinyume na maaagizo ya Rais Samia Suluhu Hassan.


“Tunazo taarifa kuwa kuna kikosi kazi kimeundwa kinazunguka humu ndani (Kariakoo) pamoja na kazi nzuri inayofanywa katika kukusanya kodi lakini Rais Samia Suluhu Hassan alikemea suala la kikosi kazi (task force),”amesema.


Aidha, Majaliwa amemuagiza Kamishna wa makusanyo ya ndani kusitisha kikosi kazi hicho na kama kuna ulazima, lazima Waziri wa Fedha afahamu.