Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel amesema kuwa, Serikali kupitia Wizara ya Afya imetenga hekali 90 kwaajili ya ujenzi wa kituo maalumu cha magonjwa ya mlipuko (isolation center) ikiwemo ugonjwa wa Marburg katika Mkoa wa Kagera kutokana na mwingiliano na wananchi kutoka nchi jirani na Mkoa huo.


Dkt. Mollel amesema hayo wakati akijibu swali la Mhe. Bernabetha Kasabago Mushashu katika Mkutano wa kumi na moja kikao cha 30, Bungeni Jijini Dodoma.