Mkuu wa Wilaya  ya Korogwe Jokate  Mwegelo  amesema kuwa Huyu ni mtoto aliokotwa katika kijiji cha Kwenangu, Kata ya Mkumbara. Alitupwa  na mama yake mzazi baada ya kuzaliwa majira ya saa 7 Usiku  nakuoneka na wanakijiji majira ya saa 1 asbh Tarehe 16/5/2023 nakukimbizwa katika kituo cha Afya Mkumbara ambapo alipatiwa matibabu na baadae majira ya saa 11 jioni alihamishiwa Hospitali ya a Wilaya ya Magunga katika Kitengo cha kuwahudumia watoto NICU ambako aliendelea kupata matibabu na sasa Afya yake imeimarika na leo tarehe 23/5/23 anapelekwa kituo cha kulelea watoto yatima Ilente kilichopo wilayani Lushoto kwaajili ya malezi. 



"Mtoto amepewa jina la Brigita Ustawi Korogwe, jina la DMO Korogwe Vijijini. 


Wakati Wanawake wengi wakiwa wanatafuta watoto wapo ambao Mungu anawabariki kupata watoto lakini wanawatupa. Niwasihi nafahamu kuna stress nyingi zinaambatana na kubeba mimba na hata malezi.