Mwanamuziki na Mwanamitandao mwenye ushawishi mkubwa wa Ghana Mona Faiz Montrage (30)  maarufu kama Hajia4reall, amepelekwa Marekani ambapo anashtakiwa kwa ulaghai wa kimapenzi uliohusisha takribani dola za Kimarekani Milioni 2.



Kampuni ya kiuhalifu aliyohusika nayo ilikuwa ikiwalenga Wamarekani wapweke wa jinsia zote na kuna wakati mwanadada huyo alijifanya kuwa yupo kwenye ndoa na mmoja wa waathirika wa ulaghai huo.


Mona anayetuhumiwa kuwa sehemu ya mtandao mkubwa wa kihalifu wa Afrika Magharibi unaolaghai watu na makampuni alikamatwa Novemba mwaka jana nchini Uingereza.


Shirika la upelelezi la Marekani FBI limeeleza kuwa Mona ameshtakiwa kwa makosa mengi ikiwemo utakatishaji fedha, njama za ulaghai na njama za kupokea pesa zilizoibiwa.



Ikiwa atakutwa na hatia hukumu yake inaweza kufikia kifungo cha miaka 20 kwa kila kosa.