Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila amefanya ziara ya Kustukiza katika Soko la Mwenge ikiwa ni mara yake ya kwanza kufanya hivyo baada ya kuhamishwa kituo cha kazi na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kutoka Kagera.
RC Chalamila akizungumza Mara baada ya kufika katika Soko hilo Leo Mei 16, 2023 amesema dhamira ya kupita kwenye maduka mbalimbali ni Kujionea hali halisi ya kinachozungumzwa na Wafanyabiashara mitaani.
"Pamoja na kuwa Sijaingia Ofisini Rasmi lakini nimeona ipo haja ya Kusikia hasa huku mtaani watu wanasema nini, lakini katika moja eneo nililopita watu wanalalamikia uwepo wa Kodi kubwa zisizoweza kulipwa na Wafanyabiashara kutokana na Kiwango kikubwa cha VAT ambayo ni asilimia 18" amesema Chalamila.


