Serikali imepokea kiasi cha TZS 6 bilioni kutoka Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) ikiwa ni sehemu ya gawio la kiasi cha Tsh bilioni 20 ambayo Benki ya NBC tumetenga kwa ajili ya wanahisa wetu kufuatia faida tuliyopata katika kipindi cha mwaka 2022. Serikali inamiliki asilimia 30 ya hisa za Benki ya NBC.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya NBC, Dk. Elirehema Doriye alikabidhi gawio hilo kwa Msajili wa Hazina Bw. Nehemiah Mchechu aliyewakilisha Serikali wakati hafla fupi ya makabidhiano hayo iliyofanyika mapema leo jijini Dar es Salaam ikihudhuliwa na wadau mbalimbali kutoka Serikali na maofisa waandamizi wa Benki ya NBC.






