Benki ya CRDB imekabidhi kwa Halmashauri ya Jiji la Arusha, Madarasa mawili katika Shule ya Sekondari ya Kalimaji yenye thamani ya Shilingi milioni 42.


Madarasa hayo yamepokelewa na Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Mhe.  Felician Mtahengerwa ambae amemuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Arusha. Mhe. John Mongela. Mhe.  Mtahengerwa ameishukuru Benki ya CRDB kwa kuendelea kusaidia jitihada za  Serikali katika kuboresha katika sekta ya elimu nchini.





Ujenzi wa madarasa hayo ni sehemu ya utekelezaji wa Sera yetu ya Uwekezaji kwa Jamii (CSI Policy) ambayo inaelekeza asilimia 1 ya faida ya benki yetu kila mwaka kuwekezwa katika miradi ya maendeleo ya jamii.