Kampuni ya Premier Bet imemtangaza mshindi George Leonard Njamasi aliyefanikiwa kushinda kiasi Cha shilingi TZS 92, 147, 650 kwa dau la shilingi 500 kwenye mpira wa miguu.
Akizungumza na waandishi wa Habari Jana Jijini Dar es Salaam, Meneja Masoko wa Kampuni ya michezo ya kubahatisha, Eric Kirita alisisitiza umuhimu wa ustaarabu kwenye michezo hiyo ya kubashiri kwani inapaswa kufanywa kama sehemu ya burudani na siyo chanzo Cha mapato.
"Ni muhimu kwa wachezaji wote ikiwa ni pamoja na George Leonard Njamasi, kufanya mambo kwa kiasi, kuweka mipaka na kipaumbele kubashiri kwa ustaarabu"
Kirita aliwahimiza wateja wake na jamii ya kitanzania kwa ujumla kutazama michezo ya kubashiri kama sehemu ya burudani ikiunda mazingira ambayo furaha inachukua nafasi kuu kuliko faida ya kifedha na kuwa michezo hii sio chanzo cha mapato.
Pia Kirita alimpongeza kwa mshindi huyo kwa kupata ushindi huo na kumshauri kuwekeza kwenye ardhi na biashara kwa uangalifu.
Kwa upande wake, Mwakilishi kutoka Bodi ya michezo ya kubahatisha Tanzania, Chiku salehe amesema.
Naye Mshindi wa mchezo wa kubahatisha, George Njamasi aliwataka wananchi wote wanaoshiriki mchezo huo, kutokata tamaa kwani fedha hizo za ushindi zitawasaidia sana kutimiza malengo yao.
Aliongezea kuwa fedha hizo zitamsaidia katika shughuli zake ambazo amejiariji.