KATIBU Mkuu Wizara ya Uchukuzi, Profesa Godius Kahyarara, amesema bado kuna fursa kubwa ya kuimarisha Bandari ya Kwala, ambayo inayotoa huduma zote za kibandari, kwani sekta ya usafirishaji ndiyo Sekta inayoongoza kwa kuleta fedha za kigeni.
Amefafanua kuwa katika kipindi cha Serikali ya awamu ya sita ongezeko limekua kwa asilimia 66.
Hayo aliyasema mwishoni mwa wiki wakati akizungumza na waandishi wa habari alipofanya ziara yake ya siku moja katika Bandari ya Kwala, ambapo alisema Rais Samia akiwa katika ziara yake nchini Zambia pamoja na Rais wa nchi hiyo, Hakainde Hichilema walikubaliana kuimarisha ushoroba wa kati kwa maana ya Reli ya TAZARA na Bandari ya Dar es Salaam.
Alisema uwepo wa Bandari ya Kwala imewarahisishia wafanyabiashara kutolazimika
kwenda katika Bandari ya Dar es Salaam kupata huduma ya usafirishaji.
“Tangu ilipotangazwa kwamba Zambia itakua sehemu ya Wana Jumuhiya katika Bandari hii ya Kwala, tumeona maombi ni mengi sana kwa njia zinazotuzunguka, wanaona faida ya kuwa katika Bandari hii kwani ni Kavu, lakini inatoa huduma zote za kibandari”
“Mfumo huu hauna ulazima wa kufika Bandari ya Posta, bali ukifika Kwala unamaliza na unarudi unapokwenda”
Prof. Kahyarara alisema Bandari ya Dar es Salaam ina wateja wengi sana ambapo meli wanazopokea hivi sasa hazijawahi kupokelewa huko nyuma, lakini changamoto kubwa ni muda wa kuzihudumia kwani meli nyingi zinasubiria kuingia kuhudumiwa.
Kadhalika Prof. Kahyarara alisema Serikali ya awamu ya sita imekamilisha Bandari mpya ya Mtwara ambapo imeweka vifaa vya kisasa vya kutelemsha Makasha hivyo wananchi wametakiwa kuchukua kama fursa
kuitumia Bandari hiyo kwani haina msongamano wa usafirishaji bidhaa.
“Kuna fursa kubwa ya kuitumia Bandari ya Mtwara, kwa mfano watu wa Malawi, ni rahisi sana kutoka Malawi ukitokea Bandari ya Mtwara na Bandari hii haina foleni,”alisema.
Aliongeza kuwa Mipango ya serikali ni kuhakikisha kwamba katika maziwa makuu pamoja na ziwa Nyasa, wanaimarisha usafiri kwani tayari kuna meli 2 za mizigo katika ziwa nyasa, Meli ya abiria MV Songea na MV Ruvuma.
Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi mkuu wa Bandari, Meneja Miliki Mamlaka ya Bandari Tanzania




