Na Beatrice Kaiza
SERIKALI imeweka wazi kuwa imejidhatiti kuboresha ulinzi na usalama katika Jiji la Dar es Salaam ili kuwezesha ufanyaji wa biashara kwa saa 24 na hivyo kuongeza mapato ya nchi katika ukuaji wa uchumi wa jiji hilo na taifa kwa ujumla.
Hayo yamebainishwa leo Novemba 06, 2023 Jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari katika uzinduzi wa duka la vifaa vya umeme la Hisense , Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Edward Mpogolo, amesema kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suruhu Hassani ameifungua nchi na kuifanya kuwa sehemu salama ya kufanya uwekezaji.
“Duka la Hisense litakuwa linauza vifaa vinavyoendana na Teknolojia ya kisasa jambo ambalo litasaidia kuwa na bidhaa Bora Tanzania”, amesema Mpogolo.
Pia amesema kuwa wafanyabiashara na wamiliki wa maduka katika jiji hilo kuhakikisha kuwa wanaboresha maandari ya maeneo yao ili kusaidia katika kulipendezesha Jiji hilo na hivyo kuvutia uwekezaji zaidi na kuongeza muda wa kuwa maduka wazi hadi ambapo wafanyakazi watakuwa wanaweza kwenda kununua vitu hadi mida ya usiku.
Aidha amesema kuwa Hisense ni wafanyabiasha wazuri ambao wamekuwa wakifanya kazi zao kwa weledi uku wakiwa na jukumu lao kuliongezea kipato Taifa.
Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya mauzo ya nje Kusini mwa Afrika kutoka Kampuni ya Hisense Hale Liu ameishukuru Serikali kwa kuweka mazingira bora ya uwekezaji na ufanyaji biashara nchini huku akisisitiza kuwa wataendela kutoa huduma bora na zinazokidhi matakwa ya wateja wao.





