Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amezitaka hospitali zote za halmashauri nchini kuwapima ugoniwa wa selimundu watoto wote wanaozaliwa katika hospitali hizo ili kujua hali zao mapema na kuanza matibabu.
Waziri Ummy ameyasema hayo wakati akizindua kampeni ya kuelimisha jamii juu ya magoniwa yasiyoambukiza yaliyofanyika katika Hospitali ya Sinza Palestina jijini Dares Salaam.
"Waganga wakuu wa mikoa mkalisimamie hili nataka hospitali zote za halmashauri chini ndani ya miezi sita zipime ugoniwa wa selimundu kwa watoto wanaozaliwa katika hospitali hizo kabla sijashuka vituo vya Afya," amesema Waziri Ummy.
