JamiƬ imehamasishwa kushiriki katika Tamasha la
Maendeleo la kutangaza Fursa za Kiuchumi na
Kupinga Ukatili (ZIFIUKUKI) lenye lengo la kuileta
Jamii sehemu moia kupata elimu na huduma
mbalimbali za kiiamii.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na
Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima ametoa
rai hiyo wakati akizungumza na waandishi wa Habari
jijini Dar Es Salaam ambapo
amesema Tamasha hilo litafanyika kwenye Mikoa
mbalimbali nchini (imetajwa).
Dkt. Gwajima amesema jukumu la kuzuia vitendo vya
ukatili ni la kila mwanajamii na kila taasisi hivyo
Wizara inashirikiana na Wadau mbalimbali kuelimisha
jamii kupinga ukatili na kufikia fursa za kiuchumi ili
kutokomeza umaskini ambapo pia huchochea ukatili.
Aidha ameiomba Ofisi ya Rais- TAMISEMI kupitia
viongozi wa mikoa husika kulipokea Tamasha hili na
kuwaelekeza Maafisa Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii kushiriki kuratibu Matamasha hayo katika
Mikoa na Halmashauri.
