Waziri wa Habari,Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe.Nape Naunye ametoa salamu akiwa njiani kuelekea Jimboni kwake Mtama na Kumpongeza Mbunge wa Jimbo la Mkuranga pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga na Wataalamu wote katika jitahada wanazopiga za kuleta maendeleo kwa Wananchi.


Mhe.Nape ameto kiasi cha shilingi million moja kwa ajili ya ujenzi ofisi ya Chama CCM Ngazi ya Kata ya Mwandege na kuahidi kuleta ujenzi wa darasa la Mafunzo ya Tehama kwa vitendo katika shule ya Sekondari Mwandege.

Aidha ametolea ufafanuzi juu la swala zima la changamoto ya mawasiliano na kusema tayari kuna team kazi maalumu ambayo ishaandaliwa kwa ajili ya kuja kufanya utafiti na pia Wilaya ya Mkuranga ipo katika Mpango maalumu utakaoanzishwa wa Mawasiliano ya 5G katika maeneo ya Viwanda ambao utarahisishwa shughuli za Tehama katika viwanda hivyo.