KAMPUNI ya michezo ya kubashiri nchini Betika yakabidhi rasmi zawadi ya Mshindi wa droo ya promosheni ya "Mbeng'o zitafunguka" kwa Mshindi wa Daladala Anselm Manga kutoka Mkoani Dodoma.



Akizungumza na waandishi wa habari leo wakati wa Makabidhiano hayo Septemba 08,2023 Afisa Habari wa Betika.

Rugambwa Juvenalius amesema Kampuni hiyo imekuwa ikiendesha promosheni mbalimbali na kuanzia mwezi Agosti ilitambulisha rasmi promosheni ya "Mbeng'o zitafunguka " kwa miezi miwili.



Aidha, amesema droo hiyo ilitoa nafasi kwa mshiriki atakaeshinda kuweza kushinda zawadi ya Bodaboda na milioni 3 kila wiki na kiasi cha milioni 2.5 kwa watu watano kila siku na zawadi kubwa kabisa va daladala mwisho wa mwezi.