Na Beatrice Kiaza
Bingwa show msimu wa pili, Vijana taklibani 24 wenye ushawishi mtandaoni rasmi wameingia kwenye kinyang'anyiro cha kumpata mshindi wa kipindi cha Bingwa msimu wa pili ambapo watakaa kwenye nyumba maalum kwa siku 72.
Akizungumza na waandishi wa habari Meneja Masoko wa Kampuni ya Startimes David Malisa amesema kuwa Tv3 ndani ya kisimbuzi cha Startimes itakuwa inaonyesha live maisha ya vijana hao.
“Zile drama, furaha, vilio basi vitatawala mjengoni yote ni kukupa burudani na elimu wewe mtazamaji wetu washiriki wa Bingwa show season 2 waaga na ndugu na jamaa na kwenda kuaza maisha ndani ya mjengo vijana wapo 24 ni wasichana na wavulana sisi kama Startimes tumewapa kwa kila vijana kisambuzi cha Startimes ili kwa ndugu zao kuangalia live kupitia tv 3,” amesema Malisa.
"Kwanza tumetengeneza ajira kwa vijana kuonyesha uwezo wao, pia kila mshiriki kila siku atakuwa anaingiza fedha kwa siku atakazokuwa anakaa ndani, na za ziada atapata kwa kushinda chalenji ambazo zinafanyika" amesema Malisa
Kwa upande wa Msimamizi mkuu wa vipindi wa kituo cha luninga cha Tv3, Emmanuel Sikawa amesema kati yao 12 ni wanawake na wengine wanaume ambao watapata fursa ya kujifunza mambo mbalimbali.
"Bingwa show imesaidia vijana mbalimbali katika masuala ya elimu, afya ya akili, kujitegemea na kutatua changamoto katika maisha yao ya kila siku," amesema Sikawa.
Pia ameongezea kuwa Inawasaidia vijana hawa 24 kupata mitaji kuendeleza biashara zao, ndoto zao katika maisha,"Sikawa.
Aidha vijana hao ni watu wenye ushawishi kwenye mitandao na hivyo elimu ambayo wataipata itaweza kuwasaidia vijana wengine kuwa mfano wa mambo yanayofaa kwenye jamii.
"Kupitia Bingwa msimu huu washiriki watapata nafasi ya kujifunza mambo mbalimbali kama elimu ya ujasiriamali, elimu juu ya matumizi mabaya ya dawa
za kulevya, matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii," amefafanuaSikawa.Sikawa amesema jumla ya vipindi
65 vitarushwa kuanzia Jumapili hadi Ijumaa kuanzia saa 4 usiku pia kutakuwa na kipindi cha nusu saa kikijulikana kama Bingwa highlight ambacho kitajumuishamatukio yote muhimu.








