Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amesema Wizara a Afya imepokea nakala ya barua ya wazi tarehe 21.07.2023

iliyoandikwa na Wawakilisi wa Madaktari waliohitimu mafunzo ya utarajali (Interns), iliyoelekezwa kwa Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, ikiwa imeainisha hoia kadhaa zinazohusu malalamiko juu ya mitihani ya usajili kabla na baada ya utarajali inayotolewa na Baraza la Madaktari Tanganyika (MCT).





Ummy amesema kufuatia malalamiko hayo ameamua kuunda Kamati huru ya chunguzi yenye Wajumbe 13 ikiongozwa na Prof. Muhammad Bakari (Manga Mkuu wa Serikali Mstaafu) ambaye atakuwa

Mwenyekiti wa Kamati ambapo Kamati hiyo itafanya kazi kwa kipindi cha mwezi mmoja na kufuata hadidu za rejea zilizoainishwa na Wizara ili kuchunguza msingi wa malalamiko yaliyotolewa a Madaktari tarajali katika barua yao na itatoa mapendekezo yatakayopelekea kutatuliwa kwa changamoto zitakazobainika.




"Katika muda wote ambao Kamati itakuwa inatekeleza majukumu yake, taratibu nyingine za mafunzo ya watarajali zitakuwa zinaendelea kama ilivyoainishwa kwenye sheria, Watarajali wenye changamoto tofauti na hii au inayoendana na hi tunawashauri wawasilishe changamoto hizo kwa

Baraza la Madaktari ili kupata msaada zaidi"


"Nihitimishe kwa kuwasihi Madaktari taraiali wawe na subira katika kipindi hiki ambacho Kamati itakua inafanya uchunguzi na pale watakapohitajika kutoa maelezo mbele ya Kamati watoe ushirikiano unaostahili, aidha niwahakikishie kuwa, Wizara itasimamia haki na ustawi wa taaluma ya Madaktari nchini"