Na Beatrice Kaiza


Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) limekuja na kampeni iliyobeba mambo nane katika kuhakikisha inakusanya madeni hayo ikiwemo kuwatangaza kwenye vyombo vya habari.

Mpaka sasa shirika hilo linawadai wapangaji wake

Sh23 bilioni fedha ambazo imeelezwa kama wangezipata zingeweza kufanyia shughuli mbalimbali za shirika ikiwemo ujenzi wa nyumba.

Akizungumza leo Jumanne Agosti 15, 2023 Kuhusu kampeni hivo illivobeba kaulimbiu va ' Lipa madeni yako kwa maendeleo ya Shirika na Taifa Letu', Meneja Habari na Uhusiano wa NHC, Muungano Saguya amesema hatua hii ni baada ya kuelekea kuisha kwa miezi mitatu aliyoitoa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati akitoa hoja ya kuahirisha kikao cha bunge Julai 2023 ambapo aliagiza wadaiwa wote wawe wamelipa madeni yao ndani ya miezi mitatu.

"Wadaiwa sugu watakaokaidi maelekezo ya shirika watakuwa wameruhusu shirika kuwatangaza katika vyombo vya habari ili mashirika na kampuni nyingine yasingie kwenye makubaliano ya kibiashara na mtu au kampuni inayodaiwa, "amesema.


Ameongeza kuwa ili kuweza kukusanya madeni katika kampeni hivo shirika limemua kufanya mambo nane ikiwemo kundwa kwa menejimenti ambayo itaanza kazi rasmi wiki hii ya kufuatilia madeni hayo.

Pia aliongezea kuwa (NHC) limeingia makubaliano na waratibu wa taarifa sahihi za waombaji wa mikopo 'CREDIT INFO BUREAU' na kuwapata majina ya wadaiwa sugu wasiweze kukopesheka popote katika taasisi za kifedha ikiwemo mabenki.

Amesema Shirika hilo, lina dai jumla ya sh bilioni 23 kutoka kwa taasisi za serikali na wat binafsi ambapo kuna wapangaji sugu 3,000 ambao wameshawasilsiha taarifa zao kwenye 'Credif Info Bureau' kwa hatua za awali na wamewapa notisi ya mwezi mmoia kulipa madeni vao kabla hawajawatangaza hadharani